Kijiwe cha usomaji kwa watoto

Usomaji kwa watoto ni shughuli mojawapo  katika mikakati ya taasisi yetu Kuelekea kuwa na maktaba ya jamii. Hivyo basi mwaka jana tuliadhimia tuanzie nyumbani ambapo tulikuwa na kijiwe cha usomaji eneo la Mikocheni A. Mtaa wa Michungwani , tulikuwa tunakusanyika pamoja na watoto walioko mashuleni na majumbani kila Jumatano na Jumamosi kwa ajili ya kujisomea kwa maana ya maktaba ya watoto.

IMG_1138

Shughuli tulizozifanya ni pamoja na:
  • Tulitembelea majumbani kuwaelezea wazazi na watoto  uwepo na umuhimu wa hiki kijiwe cha usomaji,

Tulisoma vitabu, Tulifanikiwa kusoma vitabu vingi kama vile;

1. Mlima wenye dhahabu  

2. Kunguru mvuvi hodari

3. Ndoto ya Lulu

4. Mama mbeku

 5. Nyamanza Ndege wa Amani

6. Nyani Mtu

7.Simu ya Mwanambweha

8. Jogoo na Kanga

9.  Mtoto Aliyetelekezwa

10. Nora na Matunda ya Ajabu

11. Majivuno Yamuua Samaki  

12. Sisimizi Amuua Tembo

  • Maigizo kutokana na dhima na ujumbe, ktk usomaji wa vitabu,
  • Tulijadili kitabu,

Tuliibua mijadala baada ya kusoma kitabu , kuvaa uhusika wa mwamdishi wa kitabu , na wahusika wa kwenye kitabu, kuoainisha hali halisi ya jamii.

  • Michezo mbalimbali , ya shule na ya kubuni,

Tulicheza mpira wa miguu, mpira wa mikono ,michezo ya kubuni  mingine ni  kwa ajili ya  kuweka uelewa na kumbukumbuku kwa vile tunavyovifanya

  • Tulichora kuhusiana na kitabu,

Tulichora picha na maumbo mbali mbali kutokana na picha za kwenye vitabu tulivyosoma,  na  picha za kubuni kutokana na hadithi, mfano kitabu cha” Mama Mbeku” watoto walijaribu kuchanganya rangi, ” Nora na Matunda ya Ajabu” walichora matunda mbalimbali,

  • Tulibuni hadithi nyingine kuhusiana na hadithi husika,

Watoto  walibuni  hadithi  zao wenyewe, hadithi kutokana na kichwa cha habari cha hadithi , hadithi kutokana na ujumbe , muendelezo wa hadithi kwa kupokezana.

  •   Mpira ni wa nani,

Ni shughuli  ambayo lengo kuu ni  kuleta ushirikiano,umiliki wa kijiwe  ambapo ilianza kwa kutengeneza mpira kwa pamoja na kuutumia kwa kucheza  na kuutunza

  • Nyumbani kwetu,

Tulianzisha  shughuli  hii kwa lengo la kujua mazingira ya nyumbani,- background za watoto

Tulichora picha za mazingira ya nyumbani  kwa kuelezea  kila picha

tulipeana kazi za nyumbani  zilizochochea mtoto kumhoji mzazi  kudadisi na kujua zaidi kuhusu jamii yao

  • Kujiwezesha/uwezeshwaji,

Tullisaidia katika kujiwezesha – kuchagua kitabu cha kusoma kwa pamoja watoto walichagua wawezeshaji ambao walikuwa viongozi kwa kila  kipindi  wawezeshaji waliochaguliwa  walisimamia na kusoma  kuuliza maswali, k itabu kieleweke kwa kila mmoja

  • Ufahamu  utungaji, ufupisho,maswali na majibu

Baada ya kusoma vitabu  tulitunga hadithi kutokana na uelewa wa hadithi tulizosoma, tulifupisha /muhutasari wa hadithi,  tulisomeana imla ktk kipengele kimojawapo cha hadithi, tuliulizana maswali ya ufahamu baada  ya kusoma hadithi katika kukazia uelewa.

Kijiwe cha usomaji kwa watoto 2014

Kwa mwaka huu tumepanga zoezi hili lishirikishe watoto kutoka sehemu mbalimbali, hivyo basi kama wewe ni baba,  mama, dada, kaka tunakuomba uwahimize watoto na wadogo kuja kusoma na wenzao!

Muda: Jumamosi saa 9 alasiri mpaka saa 11 jioni.