Majadiliano ya kitabu cha Kolonia Santita

Taasisi ya usomaji na maendeleo – Soma inapenda kukutaarifu kwamba, kesho tarehe 24/03/2017 siku ya Ijumaa kuanzia saa kumi kamili jioni, kutakuwa na majadiliano ya kitabu cha Kolonia Santita cha Enock Maregesi. Kolonia santita ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na dawa za kulevya. Inazungumzia vita kali kati ya Tume ya dunia ya umoja wa mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya na ugaidi wa kimataifa dhidi ya shirika kubwa la dawa za kulevya la Kolonia Santita.

Majadiliano hayo yataongozwa na mwandishi wa kitabu ndugu Enock Maregesi ambaye pia ameshiriki na kushinda tuzo ya fasihi ya kiswahili maarufu kama Mabati Cornell mwaka 2015.

Kitabu kimechapishwa na kitajadiliwa kwa mara ya kwanza hapa Soma Mkahawani mara baada ya kuchapishwa. Kama hujapata nakala yako usihofu kwani nakala zinapatikana soma book shop.

Ikiwa una swali au hoja, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa namba: 0673014071