Mzunguko wa pili wa shindano la fasihi, Andika na Soma 2013 unaanza na uchaguzi shirikishi wa dhamira. Ilipendekezwa na washiriki wa mzunguko wa kwanza 2012 kuwa inafaa washiriki wapate zaidi ya dhamira moja ya kandikia hadithi. Washindi 7 walioshiriki warsha ya uandishi wa hadithi fupi alialikwa kupendekeza dhamira  zinazowashughulisha zaidi vijana wa leo. Walipekeza dhamira zifuatazo:

Mapambano dhidi ya umasikini;

Matatizo ya madawa ya kulevya kwa vijana;

VVU na UKIMWI;

Mahusiano ya mapenzi na ngono katika umri mdogo;

Dhima ya wanaume katika jamii;

Uwelewa wa masuala ya jinsia miongoni mwa vijana

Kama wewe ni mwanafunzi wa sekondari, shiriki kwa kukubali mada mojawapo au kupendekeza nyingine.  Kama wewe si wanafunzi, shiriki kwa kupanua mjadala huu ili kupanua mawanda ya maoni na mitazamo kwa wanafunzi wa sekondari ambao ndio washiriki wa shindano hili. Mchakato wa uchaguzi wa dhamira utafungwa mnamo Machi 15 2013 na Tangazo la shindano litakuwa hewani kuanzia tarehe 1 Aprili.

Karibu ugani….