Kinyang’anyiro cha kumpata mshindi wa shindano la kuandika hadithi fupi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini – Andika na Soma, linaloendeshwa na taasisi ya usomaji na maendeleo – Soma chini ya udhamini wa ubalozi wa Denmark  kimefanyika mwishoni mwa wiki tarehe 14/10/2016.

Katika tukio hilo mwanafunzi Eliana Ludovick Swai wa shule ya sekondari ya wasichana Kifungilo iliyoko Lushoto mkoani Tanga aliibuka mshindi kwa kuwabwaga wenzake 107 waliowasilisha hadithi zao, na 20 walioingia kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mshindi; hivyo kujinyakulia kitita cha shilingi laki tano (500,000/=) na vitabu vyenye thamani ya shilingi laki tano.

Mashindano ya mwaka huu yalidhaminiwa na ubalozi wa Denmark.

Akizungumzia ushindi wake katika hali ya furaha na kutokuamini  Eliana amemshukuru sana Mungu, na walimu wake kwa kumjengea uwezo na hatimaye kuibuka mshindi. pia ameahidi kuendelea kujituma zaidi ili kuhakikisha anafika mbali.

Nafasi ya pili imeenda kwa Maria Makasi kutoka Jangwani sekondari na Seif Ibrahim Chekanae wa Tambaza sekondari zote za jijini Dar es salaam. washindi hawa wamejinyakulia zawadi ya kitita cha shilingi laki tatu (300,000) na vitabu vyenye thamani ya shilingi laki tatu (300,000) kila mmoja.

Aidha nafasi ya tatu imeenda kwa Jackline Richard Kisanga wa shule ya sekondari ya wasichana Machame iliyopo mkoani Kilimanjaro na Swedi Shaury wa Makongo sekondari ya Dar es Salaam  ambao wamejishindia pesa taslimu shilingi laki moja na nusu 150,000 na vitabu vyenye thamani hiyo kila mmoja.

Katika mjadala wa jopo uliofanywa,  mwandishi  mkongwe Richard Mabala amesema  matumizi ya mitandao ya kijamii hususani facebook na whatsapp imekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana katika kukuza uwezo wao wa kubuni na kuandika kwani wanatumia muda mwingi huko. Naye mkurugenzi wa Soma Bi Demere Kitunga amesema ni muhimu kuwa na fasihi yetu wenyewe ili kukuza utamaduni wetu, kwani kupitia fasihi tutaweza kurithisha utamaduni wetu kutoka kizazi kimoja hadi kingine na tusipofanya hivyo tutaishia kufuata utamaduni wa watu wengine. Akizungumzia shindano hili, Bi Demere amesema kwamba, shindano hili linalenga kuwafungua vijana na kuwajengea uwezo wa kuwa waandishi wazuri siku za usoni.

Matumizi ya mitandao ya kijamii hususani facebook na whatsapp yamekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana katika kukuza uwezo wao wa kubuni na kuandika– Richard Mabala

Sherehe hizi ziliburudishwa na mwanamuziki Vitali Maembe na Lakini chanzi. pia kulikuwa na ushairi kutoka kwa mwanafunzi Zawadi Suleiman kutoka shule ya sekondari Tambaza.

Hata hivyo sherehe hizi zilihitimishwa kwa mkurugenzi mtendaji – Soma kuzindua mzunguko wa nne wa Shindano hili (2016/2017) wenye dhima ya ‘Utandandawazi’ na kuomba wanafunzi wa sekondari kushiriki kwa kuandika hadithi zao na kuzituma kabla ya mwezi Februari kwisha.

MZUNGUKO WA NNE

Ikumbukwe kwamba, halfa hii ilitanguliwa na warsha ya siku tano kwa wanafunzi waliofanikiwa kuingia 20 bora kwa ajili ya kuwafundisha mbinu za uandishi na kuwajengea uwezo wa kuboresha kazi zao ziweze kukubalika katika soko la fasihi. warsha hiyo iliendeshwa na walimu Elizabeth Mahenge kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Joram Nkya kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere na Mwandishi Elias Mutani.  Wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo ni Buliba Magambo kutoka Benjamin W. Mkapa sekondari, Kulwa Abdallah – Makongo, Zawadi Suleiman – Tambaza, Swedi Shaury – Makongo, Aneth Mirambo – Ruvu, Maria Makasi – Jangwani, Jackline Kisanga – Machame girls, na Asha Malolo – Zanaki.

Zaidi kuhusu Andika na Soma

 • Shindano la hadithi fupi mzunguko wa tatu: Kifungilo yaibuka kidedea

  Shindano la hadithi fupi mzunguko wa tatu: Kifungilo yaibuka kidedea

  Kinyang’anyiro cha kumpata mshindi wa shindano la kuandika hadithi fupi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini – Andika na Soma, linaloendeshwa na taasisi ya usomaji na maendeleo – Soma chini ya udhamini wa ubalozi wa Denmark  kimefanyika mwishoni mwa wiki tarehe 14/10/2016. Katika tukio hilo mwanafunzi Eliana Ludovick Swai wa shule ya sekondari ya wasichana Kifungilo iliyoko

 • Andika Na Soma: Mzunguko wa Nne

  Andika Na Soma: Mzunguko wa Nne

  Dhamira Utandawazi Utanzu Hadithi fupi au novella ya maneno yasiyopungua 1000  wala kuzidi 3000 Maneno yasiyopungua Maneno yasiyozidi Lugha Kiswahili Vigezo Mwisho wa kupokea hadithi ni tarehe 28 February 2017 TEHAMA imerahisisha mahusiano na mawasiliano na kuifanya dunia kuwa kama ‘kijiji’. Tumia lugha nyepesi, fasaha, yenye visa,

 • Warsha ya Uboreshaji Kazi Shindano la Andika na Soma Inaendelea

  Warsha ya Uboreshaji Kazi Shindano la Andika na Soma Inaendelea

  Zimesalia siku mbili kuelekea kwenye kilele cha mzunguko wa tatu wa shindano la kumpata kinara wa hadithi fupi kwa wanafunzi wa shule za sekondari Tanzania maarufu kama Andika na Soma linaloratibiwa na kuendeshwa na taasisi ya usomaji na maendeleo (Soma). Mpaka sasa washindi kumi bora wamepatikana na wanaendelea na warsha kwaajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kuboresha kazi zao za awali

 • Soma literary Competition 2013/2014 on April 2014

  Soma literary Competition 2013/2014 on April 2014

  ANDIKA NA SOMA-SHINDANO LA UANDISHI WA HADITHI FUPI Shindano la Hadithi Fupi kwa Shule za Sekondari linaratibiwa na Taasisi ya Usomaji na Maendeleo-Soma. Shindano hili hufanyika kila mwaka. Kuanzia mwaka 2014 kilele chake kitaangukia  siku ya vitabu duniani ambayo ni tarehe 23 Aprili au karibu na tarehe hiyo. Siku hii huadhimishwa duniani kote kwa matamasha ya fasihi yanayoendeshwa kwa siku