Shindano la Uandishi wa Hadithi Fupi kwa njia ya Mtandao

[fusion_text]
Je wewe ni mwandishi? Kama ndiyo, unandoto za kuandika na ungependa kuona kazi yako ikishindanishwa na kushinda? Soma Book Café inakuletea shindano la uandishi wa hadithi fupi kwa njia ya mtandao. Andika hadithi yako juu ya mada yoyote utakayoichagua ukizingatia vipengele vya fani na maudhui. Maneno yasizidi elfu moja (1000). Shindano litafungwa tarehe 15/04/2017 saa 05:59 usiku. Tuma hadithi yako kwa njia ya email kwenda info@somabookcafe.com

Lengo la shindano hili ni kuihamasisha jamii katika suala zima la ubunifu ili kukuza vipaji vya uandishi wa aina mbalimbali. Hadithi zitakazoshinda zitachapishwa kwenye tovuti yetu. Pia mshindi atatapata fursa ya kutembelea duka letu la vitabu na kuchagua kitabu cha fasihi atakachokipenda.

[/fusion_text][two_third last=”yes” spacing=”yes” center_content=”no” hide_on_mobile=”no” background_color=”#dd9933″ background_image=”http://www.somabookcafe.com/wp-content/uploads/2017/03/1.png” background_repeat=”no-repeat” background_position=”left top” hover_type=”none” link=”” border_position=”all” border_size=”0px” border_color=”” border_style=”solid” padding=”” margin_top=”” margin_bottom=”” animation_type=”0″ animation_direction=”down” animation_speed=”0.1″ animation_offset=”” class=”” id=””][/two_third]