Habari zenu marafiki na mashabiki waUsomaji

Zoezi ama shughuli zetu za usomaji katika kitongoji cha Michungwa zinaendelea kama kawaida na kila mmoja wenu anakaribishwa kushiriki kwa namna moja ama nyingine, ikiwa ni kimawazo au hata kushiriki moja kwa moja, kuchangia chochote kinachoweza kusaidia vijana hawa wachanga katika kitongoji hiki na viginevyo hapo baadaye kuweza kuujenge na kuuimarisha vizuri utamaduni huu adhimu ambao ni aghalabu sana kuonekana hasa katika vitongoji vyetu.

Tunakukaribisha sana katika shughuli zetu hizi almaarufu “vijiwe vya usomaji” kwa watoto na vijalunga (teenegers) na soon kwa vijana.

Shughuli zetu huzifanya kila Jumatano Kuanzaia Saa 8 : 00 Mchana hadi 10 : 00 Jioni japo wakati fulani hupelekea kwenda hadi zaidi ya hapo kutokana na utamu wa shughuli za Usomaji.

 

 

Dar es Salaam-20130213-00382 Dar es Salaam-20130213-00383