Taasisi isiyoya kiserikali Inayouza vitabu na kuhimiza usomaji inatafuta Mhudumu wa Ofisi. Taasisi hii inafanya shughuli zake nchini Tanzania na ofisi zake ziko  jijini Dar es salaam.

 

Shughuli za Mhudumu wa Ofisi ni kama ifuatavyo:

  1. Kufanya usafi wa ofisi, duka la vitabu na mazingira ya ndani na nje ya ofisi.
  2. Kusaidia katika shughuli za dukani kwa maelekezo ya kiongozi wake; ikiwa ni pamoja na kuhudumia wateja.
  3. Kutumwa kupeleka na kuchukua ujumbe katika ofisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufuatilia ‘orders’, kupeleka vitabu na Ankara za madai kwa wateja na kadhalika.
  4. Kufanya shughuli mbalimbali za maandalizi ya mikutano na hafla za shirika kwa maelekezo ya kiongozi wake.
  5. Kufanya shughuli nyingine zitakazojitokeza zinazolingana na ujuzi na dhima ya kazi yake.

 

Mwombaji awe na Sifa zifuatazo:awe amemaliza kidato cha nne na kupata angalau daraja la 3 au elimu inayolingana na hiyo; mwaminifu, mbunifu, tayari kufanya kazi katika timu, aweze kupangilia shughuli zake na kuzikamilisha kwa ufanisi na kwa wakati, awe mweledi wa mawasiliano na wengine. Awe na wadhamini wawili wanaoheshimika katika jamii na awe na barua ya mtendaji wa mtaa wake unaomtambulisha kama mkazi pamoja na kitambulisho cha mpiga kura. Kuwa na leseni mpya ya udereva kutamwongezea sifa.

 

Barua za maombi zenye kichwa cha habari: Maombi ya kazi ya Uhudumu wa Ofisi na viambatanisho  (nakala ya maelezo binafsi, vyeti na nyaraka husika) zielekezwe kwa:

Mwajiri, S. L. P. 4460 Dar es salaam, zitufikie kabla ya Tarehe 15/2/2013. Waliochaguliwa kwa Usaili watataarifiwa ndani ya siku tano baada ya tarehe hiyo.

Kwa mawasiliano:

+255 22 2772759

Tupo: Mlingotini Close, Kitalu nambari 53 Regent Estate, Mikocheni A

Mshahara na Marupurupu yatategemea elimu na uzoefu wa muombaji.