IMG_2440 397114_10151231804703108_966719940_n

Shindano la uandhishi wa hadithi fupi kwa shule za sekondari lililoendeshwa na Shirika la Usomaji na Maendeleo/E&D Readership and Development Agency Soma lilikamilika tarehe 7/12/2012 kwa sherehe iliyofanyika kwenye viunga vya Mkahawa wa Vitabu Soma.

Waandishi saba waliochaguliwa kwa ubora wa kazi zao, walipokea vyeti vya ushiriki wa warsha ya uandishi. Warsha hiyo ya siku tano ililenga kukuza stadi zao za uandhishi na kuwawezesha kuboresha hadithi zao ili zifikie ubora wa kuweza kuchapishwa. Vilevile, washidi wa nafasi tatu za mwanzo walipata tuzo za fedha taslimu na vitabu– kwa ajili yao binafsi na vya maktaba za shule zao.

Shindano hili ni la kila mwaka. Lina lengo la kuongeza idadi ya vitabu pendwa kwa vijana viliyoandikwa na vijana wenyewe; na kuibua ari miongoni mwa jamii ya  kujenga mazingira ari ya kujifunza daima, kwa kuanzisha, kuhimiza na kuendeleza maktaba za shule na za jamii.

Sherehe hii ya kutoa vyeti na tuzo ilipambwa na burudani mbalimbaali: ushairi, muziki, ucheshi na usomaji wa sehemu za hadithi za washindi.

Tunashukuru marafiki wa usomaji wa kitaasisi na binafsi walioshirikiana nasi kufanikisha mchakato mzima pamoja na sherehe za kilele. Tunawaalika washirika wengine kujiunga nasi kufanukisha mzunguko wa mwaka 2013. Mchakato wa shindano ni kama ifuatavyo: a) tathmini, kupanga shughuli na kutafuta rasilimali; b) kutangaza na kuhamasisha wanafunzi kushiriki; c) mchakato wa upimaji; d) zawadi e) mafunzo; f) uenezi; g) sherehe ya uhitimu na kutoa tuzo.

Makadirio ya bajeti kwa mzunguko wa 2013 ni: SH 23,500,000.00

Maendeleo yetu ni wajibu wetu sote… tunauheshimu mchango wako…

” Inawezekana Fanya Wajibu Wako” J. K. Nyerere

Soma ripoti yote hapa (PDF):
Implementation Report of Soma Annual Literary Competition Round 1 2013