Warsha ya Uboreshaji Kazi Shindano la Andika na Soma Inaendelea

Zimesalia siku mbili kuelekea kwenye kilele cha mzunguko wa tatu wa shindano la kumpata kinara wa hadithi fupi kwa wanafunzi wa shule za sekondari Tanzania maarufu kama Andika na Soma linaloratibiwa na kuendeshwa na taasisi ya usomaji na maendeleo (Soma).

Mpaka sasa washindi kumi bora wamepatikana na wanaendelea na warsha kwaajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kuboresha kazi zao za awali na kutengeneza kazi bora zaidi zenye ubora zilizosheheni mbinu zote za uandishi kifani na kimaudhui. Warsha hii inaendeshwa na wataaluma waliobobea katika tasnia ya fasihi na lugha kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam , Chuo kikuu cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere na mwandishi Elias Mutani.

Warsha imeanza siku ya jumatatu na inatarajia kuhitimishwa siku ya ijumaa masaa machache kabla ya sherehe za kumtangaza mshindi wa shindano hilo.

Picha za matukio chini zinaonesha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini walioshiriki shindano la Andika na Soma mzunguko wa tatu na kufanikiwa kuingia 10 bora wakiendelea na semina.