Wikiendi na Watoto…

Katika azma ya kujenga jamii imara hatuna budi kushiriki na kushirikiana na watoto wetu katika shughuli zinazochangia maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Storytime
Watoto pamoja na wazazi wao katika masimulizi ya hadithi – Soma.
Jumamosi ya 16/07/2016, Soma ikishirikiana na wanafunzi wa zamani “alumni” wa Chuo Kikuu cha Cape Town (UCT) ilifanikiwa kuandaa hafla ya kifamilia. Hafla hii iliwakutanisha watoto, wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya UCT.
food
Kazi na Dawa. Watoto na wazazi wakipata chakula.

Soma katika uratibu wa shughuli za watoto iliandaa michezo mbali mbali iliyowaburudisha watoto. Michezo hiyo pia iliwashirikisha wazazi wao. Kwa ujumla michezo na shughuli nzima ililenga kujenga ushiriki na mahusiano maridhawa baina ya wazazi na watoto.

african embodiment - Copy
Watoto, pamoja na wazazi wao, katika mchezo wa kutambua na kuenzi asili na UAFRIKA wao.

Wikiendi na Watoto ilifana haswa kutokana shughuli mbalimbali zilizochagiza fikra za washiriki na kuwaburudisha. Shughuli hizo zilikuwa kivutio kikuu cha siku hiyo. Miongoni mwa shughuli hizo kulikuwamo na Masimulizi ya hadithi, mchezo wa kupuliza unga (kusaka kitu kilichomo ndani ya unga) na mchezo wa kutambua na kukumbuka vitu. Pamoja na michezo hiyo watoto walipata fursa ya kuimba na kucheza mziki, kucheza mpira na kupakwa rangi kwenye nyuso zao “face-painting”.

pudding
Mtoto, Kaya, akishiriki kwenye mchezo wa kupuliza unga – akisaka hazina ilifichwa ndani ya unga huo.
african emb
Mtoto Ricarda akionesha na kuelezea utamaduni ya Wazigua Kutoka Handeni mkoani Tanga. Katika maonesho yake alizungumzia vyakula vya asili vya atu wa huko , aina ya utalii unaopatikana na namna watu wanavyosalimiana.
Mind Cap
Watoto wakishiriki kwenye mchezo wa “Kutambua na Kukumbuka”

Siku hiyo iligubikwa na nyuso zenye furaha miongoni mwa watoto na wakubwa; huku ikiacha gumzo kubwa miongoni mwa wahudhuriaji. Pamoja na shughuli za burudani, kulikuwamo pia na maonyesho ya vitabu na vifaa vya watoto.

watoto
Baadhi ya watoto katika picha ya pamoja. kutoka kushoto ni Kaya, Kalama na Natalia.
books
Meza ya nje ya maonesho ya vitabu vya watoto yaliyoandaliwa na Soma.

 

vendor
Meza ya vifaa vya watoto.