Soma yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Kivingine

Soma imetumia jukwaa lake la Gulio la 5 la Vitabu/Book Bazaar la robo ya kwanza ya 2020 lililofanyika tarehe 07/03 kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani na miaka 25 ya Mkutano wa Beijing. Kulikuwa na Kongamano, Utambaji wa Mashairi, Uzinduzi wa Vavagaa–kipindi cha TV ya mtandaoni juu ya masuala ya jinsia. Kama kawaida kulikuwa na usomaji na simulizi kwa watoto chini ya jukwaa letu la Watoto na Vitabu. Vilevile Soma ilifanya mnada wa vifaa mbalimbali, ambao bado unaendelea.

Bibi Mama and ISoma kwa  kushirikiana na Women Fund Tanzania (WFT), Tanzania Gender Networking Programme (TGNP), Msichana Initiative na TWAA (Tanzania Women of Achievement) tuliandaa kongamano la ujenzi wa tapo la ufeminist lililoshirikisha uzoefu wa vizazi vitatu. Kongamano hilo liliwashirikisha wanawake wa kada mbalimbali ili kuzungumza masuala yanayohusu mchango wa Ufeministi, umuhimu wake sambamba na mchango wa historia ya Mkutano wa Beijing katika harakati za ukombozi wa Mwanamke kimapinduzi. Majadiliano hayo wanawake yaliangazia maana ya ufeminist /Ufeminist wa kiAfrika na namna unavyoweza kuchambua mitazamo mbalimbali juu ya masuala ya kijinsia.

Vavagaa Yazinduliwa- Tulizindua studio ya kurerekodia vipindi vya Vavagaa, televisheni ya mtandaoni “online tv talkshow”itajikita katika kuibua masuala ya haki za wanawake na usawa wa jinsia kwa lugha ya kila siku kwa makundi anuai ya kijamii.

Watoto na Vitabu– Watoto 22 (wasichana 10/wavulana 12) walishiriki kwenye kona yao wenyewe ya usomaji na simulizi. Vitabu walivyosoma na kujadili uliendana na dhamira kuu ya haki za wanawake na wasichana; na usawa wa jinsia. walijadili kitabu cha Ndoto ya Upendo https://en.wikipedia.org/wiki/Elieshi_Lema

Ushairi– Watunzi na waghani wa ushairi waliwasilisha mada ya haki za wanawake na usawa wa jinsia kishairi. Watambaji walikuwa: Anna Rwelamila alighani  mashairi mawili, moja kwa kiingereza na moja kwa kiswahili, Meki alighani  mashairi matatu, mawili kwa kiingereza na moja kwa kiswahili, Salma alighani shairi kwa Kiswahili na wimbo ambao ulitumia sauti za Kiingereza na Kiswahili. Mwanachama mkongwe wa TGNP, Talaka Nyanja, alitusalimia na shairi la kushangaza kwa Kiswahili, mshairi wa  kundi la WAKA maarufu kama  Mr. Romantic alitunga shairi mbili ambazo zote mbili zilitumia maneno ya Kiingereza na Kiswahili